Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 13:51

Korea Kaskazini yazuia watali ikihofia Ebola


Picha ya maktaba ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.
Picha ya maktaba ya kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un.

Viongozi wa Korea Kaskazini wamewapiga marufuku wageni kuhudhuria mbio za kimataifa za kila mwaka maarufu kama Pyongyang Marathon ambazo zitafanyika mwezi Aprili kutokana na hofu ya virusi hatari vya Ebola, waandalizi wamesema haya siku ya Jumatatu.

Nchi hii ambao haijapata kuwa na kisa hata kimoja cha Ebola, ilifunga mipaka kwa watalii mwezi Oktoba na kuweka masharti makali ya karantini kwa wageni kama vile wanadiplomsia na wafanyakazi wa kigeni wanaoingia nchini humo.

Nick Bonner wa kampuni ya kusafirisha wageni ya Koroyo Tours yenye makazi mjini Bejingi Uchina, ameviambvia vyombo vya habari kwamba wamearifiwa kuhusu marufuku hiyo siku ya Jumatatu. Anasema kampuni yake pekee ilikuwa inapanga kuwapeleka watali 400 kuhudhuria mbiyo hizo.

.

XS
SM
MD
LG