Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 08:04

Kismayo yadhibitiwa na majeshi ya Somalia


Mvulana akiongoza kundi la wanamgambo wa ki-Islam la al-Shabab wakati wa mazoezi ya kijeshi huko Mogadishu
Mvulana akiongoza kundi la wanamgambo wa ki-Islam la al-Shabab wakati wa mazoezi ya kijeshi huko Mogadishu

Al-Shabab kuupoteza mji huo ni pigo kwao lakini wameapa kulipiza shambulizi kutoka nje ya mji wa Kismayo

Majeshi ya Somalia yameingia katika mji wa Kismayo siku mbili baada ya kundi la wanamgambo wa al-Shabab ku-utelekeza mji huo.

Mashahidi waliithibitishia Sauti ya Amerika-VOA, Idhaa ya Kisomali kuwa majeshi ya serikali yaliingia Kismayo Jumatatu na kuchukua udhibiti wa vituo vya zamani vya al-Shabab.

Wakazi walionekana kuyakaribisha majeshi. Baadhi ya wizi wa mali uliripotiwa kutokea baada ya kundi la al-Shabab kuwaondoa wapiganaji wake waliobaki Jumamosi.

Kundi hilo la wanamgambo wa ki-islam liliondoka mji wa Kismayo ambapo ni ngome yake kubwa ya mwisho nchini Somalia, kufuatia shambulizi moja lililofanywa Ijumaa na majeshi ya Kenya yakishirikiana na majeshi ya Umoja wa Afrika.

Al-Shabab kuupoteza mji huo ni pigo kwao ambapo wanatumia bandari ya mji wa Kismayo kuingiza silaha na kukusanya fedha kupitia kodi.

Johnnie Carson, naibu waziri wa mambo ya nje anayeshughulika na masuala ya Afrika alionya kwamba kundi la al-Shabab limepungua kasi yake lakini halijatokomezwa kabisa.

Wanamgambo hao wameapa kulipiza shambulizi kutoka nje ya mji wa Kismayo.

Majeshi ya Kenya yaliingia Kismayo mwaka jana baada ya mfululizo wa matukio ya utekaji nyara wakati wa kukatisha mpaka ambapo Kenya walililaumu kundi la wanamgambo wa al-Shabab kuhusika.
XS
SM
MD
LG