Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 22:59

Kiongozi wa upinzani wa Tunisia azuiliwa nyumbani kwake na maafisa wa serikali


Wafuasi wa upinzani nchini Tunisia wakiwa kwenye maandamano ya awali. Picha ya maktaba.
Wafuasi wa upinzani nchini Tunisia wakiwa kwenye maandamano ya awali. Picha ya maktaba.

Chama ya upinzani cha Kiislamu cha Tunisia cha Ennahdha kimesema kwamba mmoja wa viongozi wake amewekwa kwenye kizuizi cha nyumbani na maafisa wa serikali, kwa kile ambacho kimeelezewa ni uamuzi ambao ni kunyume cha sheria. 

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, taarifa iliyotolewa Jumapili na Ennahdha imelaani hatua hiyo dhidi ya Abdel Karim Harouni na kutaka aachiliwe huru mara moja.

Ushirika wa vyama vya upinzani nchini Tunisia wa National Salvation Front ambao unajumuisha Ennahdha umesema kupitia taarifa kwamba Harouni yuko kizuizini nyumani kwake tangu Jumamosi jioni, siku moja kabla ya kushiriki mkutano wa kutayarisha kongamano la chama ambalo limepangwa kufanyika Oktoba.

Hatua hiyo imekuja baada ya kiongozi wa kiislamu wa Tunisia Rached Ghannouchi kukamatwa mapema mwaka huu na kupewa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa tuhuma za kuwaita maafisa wa polisi wadhalimu, katika kile ambacho chama chake kimeelezea ni kesi ya uongo.

Ghannouchi mwenye umri wa miaka 82 ni mwanzilishi wa chama cha Ennahdha na pia spika wa zamani wa bunge, ni mkosoaji maarufu wa rais wa Tunisia Kais Saied. Kiongozi huyo amesisitiza kwamba Saied mwaka 2021 alijitwalia madaraka ambapo ni sawa na mapinduzi.

Polisi wamewazuia viongozi wengine kadhaa wa upinzani tangu mwanzo wa mwaka huu.

Forum

XS
SM
MD
LG