Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 18:23

Besigye aachiliwa baada ya kushikiliwa kwa muda


Majina yanavyoonekana katika karatasi za kupiga kura.
Majina yanavyoonekana katika karatasi za kupiga kura.

Vituo vya upigaji kura 14 nchini Uganda vitarudia upigaji kura Ijumaa. Upigaji kura uliakhirishwa kwenye vituo hivyo kwa sababu masanduku yalichomwa moto na wapiga kura waliodai yalikuwa na karatasi zilizokuwa tayari zimewekwa alama.

Wakati huo huo polisi nchini Uganda wamemwachia mgombea wa upinzani kizza besigye ambaya anampa changamoto kubwa Rais Yoweri Museveni katika uchaguzi uliofanyika Alhamis.

Akizungumza na Sauti ya Amerika-VOA wakili wa Bessigye alisema mteja wake alikamatwa alhamis jioni katika wilaya ya Nguru nje kidogo ya mji wa kampala. Wakili Hajjat Lukwago Shifrah alisema mgombea wake alibaini ushahidi wa wizi wa kura.

Karatasi zenye majina ya wagombea Feb. 18, 2011.
Karatasi zenye majina ya wagombea Feb. 18, 2011.

Awali tume ya uchaguzi nchini Uganda iliongeza muda wa kupiga kura kwa sababu kadhaa baada ya vituo vingi kuchelewa kufunguliwa. Katika sehemu moja mjini Kampala polisi walitumia gesi ya machozi kutawanya wapiga kura waliokasirika ambao walikuwa wakisubiri kwa takribani saa saba kuwasili kwa karatasiza kura na kugundua tu baadaye kulikuwa hakuna karatasi za kura ya urais.

Licha ya matatizo haya kujitokeza waganda walijitokeza kwa idadi kubwa kupiga kura katika uchaguzi wa rais na bunge.

XS
SM
MD
LG