Mrithi wake Sheikh Meshal al-Ahmad al-Sabah mwenye umri wa miaka 83, alionekana akitokwa na machozi katika sala iliyohudhuriwa na wanafamilia wa utawala ya Al Sabah na spika wa bunge la Kuwait.
Sheikh Meshal ameshikilia uongozi wa Kuwait tangu 2021, pale Sheikh Nawaf afya yake ilipodhoofika na kumkabidhi majukumu yake mengi. Jeneza la Sheikh Nawaf ambaye jeneza lake lilifunikwa kwa bendera ya Kuwait alizikwa kwenye makaburi ya Sulaibikhat, ambako wanafamilia wengine wamezikwa, baada ya sala kwenye msikiti wa Bilal bin Rabah. Alifariki akiwa na umri wa miaka 86.
Viongozi kutoka sehemu mbali mbali za dunia wametoa heshima zao kwa Sheikh Nawaf ambaye amehudumu kwenye nyadhifa tofauti kwa takriban miongo sita. Aliwahi kuwa waziri wa Ulinzi, Kazi na pia naibu mkuu wa jeshi la taifa.
Forum