Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:45

Kiongozi wa Mafia akamatwa Italy Jumatatu


Kiongozi wa mafia Messina Denaro, aliyekamatwa Jumatatu. Januari
Kiongozi wa mafia Messina Denaro, aliyekamatwa Jumatatu. Januari

Mmoja wa watu wanaotafutwa sana  nchini Italy, ambaye ni kiongozi wa kundi la Mafia Messina Denaro amekamatwa.

Shirika la habari la taifa la ANSA Jumatatu limeripoti kuwa kiongozi huyo wa Mafia tawi la Sicily, la Casa Nostra mafia amekuwa akitafuwa kwa maika 30, alikamatwa kwenye kituo cha afya binafsi mjini Palermo. Televisheni ya serikali imesema kwamba Denaro amepelekwa kwenye eneo la siri muda mfupi baada ya kukamatwa.

Kesi yake iliendeshwa bila ya yeye kuwepo mahakamani kwa mauaji ya dazeni ya vifo ikiwa ni pamoja na vifo vya waendesha mashtaka waliokuwa wakisimamia kesi dhidi ya waongoza mashitaka Giovanni Falcone na Paolo Borsellino. Denaro mwenye umri wa miaka 60 anakabiliwa na adhabu kadhaa za kifungo cha maisha.

Wakati mmoja Denaro alidai kuwa watu aliowauwa angeweza kuwajaza kwenye kaburi. Waziri mkuu wa Italy Giorgia Meloni kupitia taarifa amesema kwamba kukamatwa kwa Denaro ni ushindi mkubwa dhidi ya makundi ya kihalifu nchini humo. Septemba mwaka jana, polisi walisema kwamba licha ya Denaro kutafutwa kwa miaka 30, bado alikuwa na uwezo wa kutoa amri kwa kundi la Mafia kwenye mji wa magharibi mwa Sicily wa Trapani.

XS
SM
MD
LG