Kimbunga hicho kilichopewa jina Khanun sasa hivi kipo kwenye maji ya bahari kati ya China na visiwa vya kusini magharibi mwa Japan, kikitarajiwa kusitisha kasi na kisha kugeukia upande wa mashariki kufikia Ijumaa, kulingana na idara ya hali ya hewa ya Japan.
Hadi mvua za centimita 20 zinatarajiwa kwenye eneo la Okinawa kufikia katikati mwa Ijumaa, idara hiyo imeongeza. Kulingana na serikali ya kieneo ya Okinawa, kimbunga hicho kimejeruhi watu 41, watatu miongoni mwao wakijeruhiwa vibaya.
Maelfu ya wakazi wamebaki bila umeme hivi leo kwa kuwa kimbunga hicho kimezuia shuguli za ukarabati kuendelea. Shuguli za usafiri pia zimeathirika ingawa baadhi ya safari za ndege zinatarajiwa kurejea baadaye leo.
Forum