Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 03:43

Kiir akutana na al-Bashir Addis Ababa


Rais Omar al-Bashir wa Sudan akimkaribisha mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir kwenye uwanja wa ndege wa Khartoum October 8,2011.
Rais Omar al-Bashir wa Sudan akimkaribisha mwenzake wa Sudan Kusini Salva Kiir kwenye uwanja wa ndege wa Khartoum October 8,2011.
Rais Omar al-Bashir wa Sudan na Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini wanakutana Jumatatu mjini Addiss Ababa, Ethiopia kwa mazungumzo yenye lengo la kukamilisha mkataba wa amani kati ya nchi zao mbili .

Marais hao wanatarajiwa kujadili na kukamilisha makubaliano juu ya masuala ya mpaka, kugawanya mapato ya mafuta na usalama, na hasa suala la eneo la Abyei.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:18 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Marais hao wawili walikutana na waziri mkuu mpya wa Ethopia Hailemariam Desalgn, Jumapili na kuwa na mazungumzo ya saa mbili pamoja na wajumbe wao.

Makubaliano juu ya uchumi, mafuta na masuala ya biashara yako tayari kutiwa saini. Lakini marais hao kwanza lazima wakubaliane juu ya masuala yalosalia, anasema balozi Badredin Abdallah kutoka ujumbe wa Sudan.

“Kuna baadhi ya masuala yalosialia, ambayo bado yana utata kuhusiana na suala la usalama, kuhusu masuala ya mpaka na hata uhusiano wa Sudan Kusini katika baadhi ya mambo kuhusiana na sula la pande mbili na bila shaka watalijadili suala la Abyei.”

Sudan ilikubali ramani ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya kuwepo na eneo lisilokuwa na shughuli za kijeshi kati ya mipaka yao chini ya masharti maalum.

Msemaji wa wajumbe wa Sudan Kusini Atif Keir anasema majadiliano ya mwisho baina ya marais hao wawili hayatakuwa rahisi.

“Bila shaka tunakabiliwa na matatizo mgumu ya hapa na pale, baadhi ya masuala yalosalia wajumbe wa pande mbili wameshindwa kufikia makubaliano.”

Sudan kusini ilijitenga kutoka Sudan hapo mwaka 2011, na hivyo kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe vilvyoendelea kwa mda mrefu. Nchi hizo mbili zimekuwa na ugomvi tangu kutengana kwao, na kupelekea kutokea kwa mapambano makali baina yao mapema mwaka 2012.

Baraza la Usalama la Umoja Mataifa litaziwekea vikwazo Sudan na Sudan Kusini ikiwa zitashindwa kufikia makubaliano.
XS
SM
MD
LG