Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Oktoba 10, 2024 Local time: 22:39

Kenyatta awataka wakenya kuwatambua majirani ili kuimarisha usalama


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, akisimama na mkuu wa majeshi ya Kenya, Jenerali Julius Waweru Karangi wakati wa sherehe za sikukuu ya Mashujaa, Oktoba 20, 2013.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, akisimama na mkuu wa majeshi ya Kenya, Jenerali Julius Waweru Karangi wakati wa sherehe za sikukuu ya Mashujaa, Oktoba 20, 2013.
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya, ametowa wito kwa wakenya kuungana nae ili kupambana na ukoloni mamboleo na ushawishi wa kigeni wenye lengo la kubadili muelekeo wa nchi yao.

Akilihutubia taifa katika kuadhimisha sikukuu ya Mashujaa iliyofanyika Jumapili, Rais Kenyatta alisema taifa linabidi kuheshimu na kuendelea na vita vya mashujaa wa nchi waliopigana dhidi ya ukoloni na vikosi vya kibeberu.

Wakati huo huo Kiongozi huyo amewataka wakenya kuwatambua na kuwajuwa majirani zao na kila kinachotendeka karibu na makazi yao kama njia ya kuimarisha usalama wa nchi hiyo.

Akigusia suala la waathiriwa wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa kenya uliofanyika mwaka 2007, Rais Kenyatta alisema wakazi wote waliopoteza makazi yao wamepatiwa makazi mapya. Hata hivyo watu waliopoteza makazi yao wanasema hawawezi kutumia mashamba waliopewa kwa vile hayana rutuba na wamerudi katika makambi ya Naivasha.
please wait

No media source currently available

0:00 0:03:43 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizungumza na Sauti ya Amerika, Steven Mmbugua, mwakilishi wa watu waliopoteza makazi yao wanaoishi katika makambi mjini Naivasha, anasema wameridhika na juhudi za serikali mpya ya Rais Kenyatta lakini anasema fedha walizopewa hazitoshi kununua mashamba na watu waliopewa mashamba wamerudi kwani maeneo waliopewa hayatowawezesha kukidhi maisha yao.
XS
SM
MD
LG