Michezo ya olimpiki mjini London inaendelea huku ikiwa imeingia katika wiki ya kwanza ya mashindano ya riadha na kuzusha wasiwasi miongoni mwa mashabiki wa Kenya kutokana na matokeo ya michezo ya kwanza kwanza – kama vile marathon wanawake na mbio za mita elfu 10 wanawake na wanaume ambapo Kenya imepata medali moja tu ya dhahabu katika mita elfu tatu kuruka viunzi na maji.
Lakini hivyo sivyo wanavyoona maafisa wa team Kenya mjini London. Katika mahojiano na msemaji wa timu hiyo Peter Angwenyi aliambia VOA kuwa Team Kenya inafanya vizuri na mpaka hadi wiki ya kwanza ya mashindano ya riadha haijapoteza hadi medali moja iliyopata Beijing mwaka 2008.