Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 19, 2024 Local time: 15:20

Kenya yachukua hatua kali dhidi ya watengenezaji pombe ya kiyenyejiSerikali ya Kenya ilitangaza Alhamisi hatua kali dhidi ya watumishi wa serikali wanaohusika na kazi za kudhbiti pombe haramu ya kiyeneji na kufunga kampuni kuu ya kupika pombe hiyo nchini humo.

Waziri wa mambo ya ndani Joseph Ole Lenku alitangaza Alhamisi kwamba watumishi 52 wa idara mbali mbali za serikali na wakuu wa Mamlaka ya kudhibiti Ulevi na Madawa ya kulevya NACADA wamesitishwa kazi.

Bw Ole Lenku amesema mkurugenzi mkuu wa NACADA Dr. William Okedi na mkuu wa idara ya kupambana na bidhaa za bandia ndio wanaohusika na kuweka viwango na kanuni za biashara hiyo, lakini inaonekana anaema hawakufanya kazi za na hivyo wamesitishwa kazi.
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:34 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mwenyekiti wa NACADA John Mututho akizungumza na Sauti ya Amerika Alhamisi amesema ni jambo la kusikitisha na watapeleka maafisa wa afya kote nchini kukagua na kuchunguza biashara ya pombe haramu.

Mnamo muda wa wiki moja karibu watu 81 katika County 6 za Kenya wamefariki kutokana na kunywa pombe iliyotiwa kemikali ya sumu ya Menthanol. Zaidi ya watu 200 wamelazwa hospitali baadhi akipoteza uwezo wa kuona au kupoteza fahamu.
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:31 0:00
Kiungo cha moja kwa moja


Wakizungumza na Sauti ya Amerika kutoka mji wa Naivasha, baadhi ya watumiaji pombe hiyo wanasema wanalazimika kunywa kinywaji hicho cha rahisi kutokana na matatizo ya maisha na kujaribu kusahau matatizo kwa kulewa.
XS
SM
MD
LG