Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Februari 26, 2024 Local time: 11:25

Kenya na China zaimarisha ushirikiano


Rais wa kenya Uhuru Kenyatta (L) na Rais Xi Jinping wa China
Rais wa kenya Uhuru Kenyatta (L) na Rais Xi Jinping wa China
Serikali ya Kenya imetiliana saini na serikali ya China mikataba yenye thamani ya dola bilioni tano kwa ajili ya miradi ya ujenzi wa reli, nishati na ulinzi wa wanyamapori.

Mkataba huo ulitiwa saini wakati wa ziara ya kwanza ya Rais Uhuru Kenyatta huko China tangu aliposhinda uchaguzi wa mwezi Machi mwaka huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:10 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Rais wa China Xi Jinping alisema wakati wa sherehe za kutia saini kwamba Bwana Kenyatta ataweza kuiongoza Kenya kuelekea uchumi uliokamilika.

Uhusiano wa kiongozi huyo wa Kenya na nchi za magharibi unaweza ukakumbwa na matatizo kutokana na hali kwamba anakabiliwa na mashtaka huko The Hague yanayohusiana na ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Seneta Murkomen Kipchumba wa Kenya amesema mkatabu huo ni muhimu sio tu kwa Kenya bali kwa nchi za Afrika Mashariki.

Anasema mpango wa ujenzi wa njia ya reli utasaidia sana nchi za Afrika ya kati kupanuka kiuchumi na kupunguza sana msongamano wa bidhaa kwenye bandari ya Mombasa.
XS
SM
MD
LG