Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 04, 2022 Local time: 01:12

Kenya kukata rufaa juu ya uamuzi wa ICC


Watuhumiwa watatu wa ghasia za baada ya uchaguzi

Jopo la majaji wa ICC liliamua kwamba serikali ya Kenya haijatoa ushahidi wa kuwashitaki watuhumiwa wa ghasia za uchaguzi

Kenya imesema inampango wa kukata rufaa uwamuzi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC ulotupilia mbali ombi la serikali kutaka kesi za watuhumiwa sita wa ghasia baada ya uchaguzi kufanyika Kenya.

Jopo la majaji wa ICC liliamua Jumapili kwamba serikali ya Kenya haijatoa ushahidi wa kutosha kwamba inafanya uchunguzi au kuwafungulia mashtaka watuhumiwa ambao wanalaumiwa kupanga ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2008.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne , mwanasheria mkuu wa Kenya Amos Wako amesema anashangazwa kwamba majaji wa ICC wamefikia uamuzi huo bila ya kuwasikiliza mawakili wa Kenya.

Amesema atakutana na mawakili wa serikali mjini London Ijumaa akiwa na mtazamo wa kukata rufaa juu ya uamuzi huo.

Ghasia za baada ya uchaguzi na zile za kikabila huko Kenya ziliuwa takriban watu 1300 na kukosesha makazi maelfu ya watu.

Watuhumiwa sita wanaolaumiwa kwa kupanga na kufadhili ghasia ni pamoja na wanasiasa mashuhuri na wafanyabiashara. Katika taarifa yake mwanasheria mkuu wa Kenya anasema anaimani kwamba afisi ya rufaa ya ICC itapata habari kamili juu ya maendeleo ya uchunguzi dhidi ya watuhumiwa hao sita.

XS
SM
MD
LG