Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, kiwanda hicho ndicho kikubwa zaidi barani Afrika, kilichojengwa kwenye peninsula iliyopo nje ya mji mkuu wa kibiashara wa Lagos, kwa gharama ya dola bilioni 20, kikimilikiwa na tajiri mkubwa sana katika bara hilo, Aliko Dangote.
Ingawa Nigeria ndiye mzalishaji wa juu wa mafuta barani Afrika, imekuwa ikitegemea mafuta kutoka mataifa ya nje. Kiwanda cha Dangote sasa kitaiwezesha Nigeria siyo tu kujitegemea, mbali pia kuuza mafuta kwenye mataifa jirani ya Afrika Magharibi, na hatimaye kubadili biashara ya mafuta katika ukanda wa Atlantiki.
Maafisa wa kampuni hiyo wameiambia Reuters kwamba kitaanza majaribio ya wiki hii, baada ya kupokea shehena ya 6 ya mafuta ghafi hapo Januari 8.
Forum