Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:47
VOA Direct Packages

Kampeni za urais zapamba moto Nigeria siku chache kabla ya uchaguzi kufanyika


Kuta zilizojaa mabango ya wagombea viti kwenye uchaguzi ujao wa Nigeria
Kuta zilizojaa mabango ya wagombea viti kwenye uchaguzi ujao wa Nigeria

Wagombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu wa Nigeria uliobakisha wiki moja kufanyika, Jumamosi wameendelea na kampeni zao kote nchini kwa lengo la kujizolea kura zaidi.

Zaidi ya wapiga kura milioni 90 wamejiandikisha kushiriki zoezi hilo, wakati rais aliyeko madarakani Muhammadu Buhari akikamilisha muda wake wa mihula miwili kwa mujibu wa katiba. Akiwa juu ya basi lisilokuwa na paa, mgombea wa chama tawala cha All Progressive Congress Bola Tinubu alifanya kampeni zake kwenye barabara za mji wa Maiduguri kaskazini mwa jimbo la Borno, wakati akitarajiwa kukamilisha kampeni zake mjini Lagos hapo Jumanne.

Kwenye jimbo jirani la Adamawa, mgombea maarufu wa upinzani Atiku Abubakar kutoka chama cha People’s Democratic Party alifanya kampeni katika mji wa Yola, wakati pia akiwa kwenye basi maalum la kampeni lenye ghorofa mbili. Ingawa mgombea huru Peter Obi hakuwa kwenye kampeni moja kwa moja, alifanya kampeni zake kupitia kwenye mitandao ya kijamii akiomba wafuasi wake kote nchini wampigie kura.

Kampeni hizo zinaendelea wakati Nigeria ikikabiliwa na uhaba wa fedha baada ya benki kuu kupiga marufuku noti za awali na kubuni mpya mwezi Decemba. Tatizo hilo limepelekea maandamano katika baadhi ya miji huku wateja wakishambulia mabenki na kufunga barabara siku chache tu kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.

XS
SM
MD
LG