Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Mei 28, 2024 Local time: 03:25

Kambi za wakimbizi Kenya kufungwa mwezi huu


Wakimbizi katika kambi ya Daadab nchini Kenya
Wakimbizi katika kambi ya Daadab nchini Kenya

Tangu ghasia za uchaguzi wa 2007, serikali inajitahidi kutoa makao mapya kwa waathiriwa wa ghasia hizo aidha kuwapatia fedha za kujenga na kununua mashamba mapya baada ya kufurushwa makwao.

Kulingana na Serikali ya Kenya, kambi zote za wakimbizi wa ndani walioathiriwa na ghasia za uchaguzi wa mwaka 2007 sasa zitafungwa mwezi wa kumi na hususan kabla ya kuanza kwa mvua ya El NINO nchini Kenya.

Naibu wa Rais wa Kenya William Ruto, amesema kambi zote za wakimbizi wa ndani walioathiriwa na mapigano na ghasia za uchaguzi wa mwaka 2007 zitafungwa katika muda wa wiki moja ijayo kutokana na hatari ya mvua ya El Nino inayotarajiwa kunyesha wakati wowote hivi sasa.

Tangu ghasia za uchaguzi wa 2007, serikali inajitahidi kutoa makao mapya kwa waathiriwa wa ghasia hizo aidha kuwapatia fedha za kujenga na kununua mashamba mapya baada ya kufurushwa makwao.

Lakini kuna maelfu ya wakimbizi wa ndani ambao bado kufarijiwa na serikali licha ya masaibu wanayopata.Wengi wamekuwa wakiandamana barabarani kudai haki yao.

Lakini sasa Naibu wa Rais William Ruto anasema kuanzia juma lijalo, kambi hizo zitafungwa.

Lakini licha ya uamuzi huo wa serikali, kuna idadi kubwa yawakimbizi wa ndani wanaodai kuwa hawajapata chochote kutoka kwa serikali tangu uchaguzi huo karibu miaka saba iliyopita.

Wanasiasa wa upinzani wamekuwa wakilalamika kuhusu kubaguliwa kwa baadhi yawakimbizi wa ndani hasa katika maeneo yanayo-thibitiwa na upinzani.

XS
SM
MD
LG