Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 19:13

Kambi ya jeshi yashambuliwa Kinshasa


Hii sio mara ya kwanza eneo hilo kushambuliwa tukio jingine lilishatokea Disemba mwaka jana.
Hii sio mara ya kwanza eneo hilo kushambuliwa tukio jingine lilishatokea Disemba mwaka jana.

Watu wenye silaha walishambulia kambi moja ya jeshi katika mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC, Jumanne lakini serikali ya nchi hiyo inasema hali hiyo haraka ilidhibitiwa na serikali.

Katika mahojiano na Idhaa ya ki-Faransa ya Sauti yaAmerika-VOA msemaji wa serikali ya Congo, Lambert Mende alisema kundi moja dogo la washambuliaji lilijaribu kuingia kwenye kambi ya Tshatshi mjini Kinshasa lakini walizuiliwa.

Lambert Mende
Lambert Mende


Bwana Mende alisema maafisa bado hawajaelezea kama washambuliaji hao walikuwa magaidi au wezi.
Ujumbe wa maandishi kwenye televisheni ya taifa ya DRC uliwaeleza watazamaji kuwa hakukuwa na haja ya kupatwa na khofu. Mende alisema wanajeshi walikuwa wakifanya doria kwenye mji ili kuwahakikishia wananchi usalama.

Watu wenye silaha wafuasi wa mchungaji mmoja wa dhehebu la kikristo ambaye anampinga Rais Joseph Kabila walishambulia kituo hicho hicho na waliteka kwa muda mfupi kituo cha televisheni ya taifa mwezi Disemba mwaka jana. Serikali ilisema zaidi ya watu 100 waliuwawa wakati majeshi yake yalipojibu mashambulizi hayo.

Mvutano wa kisiasa umeongezeka huko DRC kufuatia tetesi kwamba Rais kabila huwenda akajaribu kubadilisha katiba na kugombea madaraka kwa muhula wa tatu katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2016.

XS
SM
MD
LG