Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 02:37

Jumuiya ya kimataifa inasifia utiaji saini wa kijeshi wa Sudan na raia


Raia wa Sudan akishikilia bendera ya nchi hiyo mjini Khartoum. April 19, 2019. REUTERS/Umit Bektas/File Photo
Raia wa Sudan akishikilia bendera ya nchi hiyo mjini Khartoum. April 19, 2019. REUTERS/Umit Bektas/File Photo

Viongozi waandamizi wa jeshi na makundi ya kiraia walikubaliana makubaliano ya kuweka msingi wa kuanzisha tena mamlaka ya kiraia hatua iliyokaribishwa na Umoja wa Mataifa, Washington, London, Brussels, Riyadh na Abu Dhabi miongoni mwa mengine

Kutiwa saini kwa makubaliano ya awali na utawala wa kijeshi wa Sudan na raia kumesifiwa na jumuiya ya kimataifa lakini wengi ndani ya Sudan wanautazama kwa mashaka makubwa.

Sudan moja ya nchi maskini zaidi duniani imegubikwa na misukosuko mikubwa tangu mkuu wa majeshi Abdel Fattah al-Burhan alipofanya mapinduzi ya kijeshi mwezi Oktoba 2021 na kuvuruga kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia.

Unyakuzi huo wa madaraka ulikuja miaka miwili na nusu tu baada ya maandamano makubwa ya mitaani kulishinikiza jeshi kumuondoa madarakani mtawala wa muda mrefu Omar al-Bashir.

Wengi walithubutu kuamini kuwa mpango wa kushirikiana madaraka ungehakikisha uhuru na kutoa haki lakini mapinduzi hayo yalizima matumaini hayo, na kuchochea wafadhili kusitisha ufadhili na kuzidisha mgogoro wa kiuchumi uliodumu kwa muda mrefu.

Matukio ya mwaka 2021 pia yamesababisha kuzorota kwa mizozo ya kiusalama katika maeneo ya mbali.

Siku ya Jumatatu viongozi waandamizi wa jeshi na makundi ya kiraia walikubaliana makubaliano ya kuweka msingi wa kuanzisha tena mamlaka ya kiraia hatua iliyokaribishwa na Umoja wa Mataifa, Washington, London, Brussels, Riyadh na Abu Dhabi miongoni mwa mengine.

Makubaliano hayo awamu ya kwanza ya mchakato wa awamu mbili yalitiwa saini na kambi kuu ya kiraia Forces For Freedom and Change ambayo kwa miezi kadhaa ilikuwa ikipinga kujihusisha na jeshi baada ya mapinduzi.

XS
SM
MD
LG