Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 04, 2023 Local time: 23:03

Jeshi la polisi Tanzania lasisitiza amani wakati wa uchaguzi


Mkutano wa kampeni za uchaguzi Tanzania

Nchini Tanzania wakati kesi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar Es Salaam ya kutaka tafsiri ya sheria juu ya umbali unaoruhusiwa wapiga kura kusimama baada ya kupiga kura haijatolewa uamuzi, jeshi la polisi nchini humo limesisitiza kwamba halitaruhusu kuwepo mikusanyiko yeyote baada ya upigaji kura kukamilika Oktoba 25 mwaka huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:12 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Jaji Sakieti Kihiyo, ambaye ni kiongozi wa jopo la majaji watatu, Alhamis aliakhirisha tena hukumu ya kesi hiyo katika shauri la kikatiba linaloleta mvuto wa aina yake nchini humo lililofunguliwa na mgombea ubunge wa viti maalum kwa tiketi ya chama cha upinzani cha Chadema, Amy Kibatala, akiomba mahakama kutoa tafsiri ya kifungu cha 104 cha sheria ya uchaguzi baada ya kauli mbalimbali za viongozi wa serikali kutoruhusu wapiga kura kukaa vituoni mara bada ya kumaliza kupiga kura huku wapinzani wakisisitiza kuwa sheria inaruhusu kukaa umbali wa mita 200.

Ernest Mangu, mkuu wa jeshi la polisi nchini humo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar Es salaam, Alhamis alisema kwamba jeshi hilo halitasita kukabiliana na watu au kikundi chochote kitakachokaidi sheria, kanuni na taratibu za uchaguzi kwa kisingizo cha kulinda kura.

Mkuu huyo wa jeshi la polisi alitaka kuwepo kwa amani na utulivu kama ilivyokuwepo wakati wote wa kampeni za uchaguzi mkuu zinazohitimishwa Jumamosi, Oktoba 24 mwaka huu

Watanzania wanatarajiwa kupiga kura Oktoba 25 mwaka huu kuwachaguwa madiwani, wabunge na rais, katika uchaguzi mkuu ambao vyama vinane vimesimamisha wagombea wa urais.

XS
SM
MD
LG