Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 20, 2024 Local time: 14:41

Jeshi la majini la Marekani lilizuia shehena ya silaha zikielekea Yemen


Mfano wa meli za jeshi la wanamaji Marekani
Mfano wa meli za jeshi la wanamaji Marekani

Taarifa kutoka meli ya marekani US 5th Fleet imesema bunduki 2,116 aina ya AK-47 zilipatikana kwenye meli ya uvuvi katika Ghuba ya Oman ambayo ilikuwa ikipita "njia inayotumiwa kihistoria kusafirisha mizigo haramu" kwenda waasi wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran

Jeshi la Wanamaji la Marekani lilisema Jumanne kwamba lilizuia shehena ya silaha za mashambulizi wiki iliyopita iliyokuwa ikielekea Yemen ambayo inaamini zilitokea Iran.

Taarifa kutoka meli ya Marekani US 5th Fleet imesema bunduki 2,116 aina ya AK-47 zilipatikana kwenye meli ya uvuvi katika Ghuba ya Oman ambayo ilikuwa ikipita "njia inayotumiwa kihistoria kusafirisha mizigo haramu" kwenda waasi wa kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Taarifa hiyo ilisema vikosi vya Marekani vilizuia meli nyingine mbili za uvuvi katika eneo moja katika kipindi cha miezi miwili iliyopita ambazo pia zilikuwa zimebeba silaha kutoka Iran kwenda Yemen.

Iran imekuwa ikikanusha mara kwa mara kuwapa silaha waasi wa kihouthi huku wataalamu huru na wa Umoja wa Mataifa wanafuatilia vifaa kutoka kwa shehena zilizokamatwa na kuzirudisha Iran.

XS
SM
MD
LG