Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 03, 2024 Local time: 23:24

Japan yaadhimisha miaka 50 ya ushirikiano na urafiki na mataifa ya ASEAN


Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida na mwenzake wa Malaysia Anwar Ibrahim wakipongeza mawaziri wao wa mambo ya kigeni baada ya kutia saini makubaliano n a mataifa ya ASEAN, Jumapili mjini Tokyo, Japan
Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida na mwenzake wa Malaysia Anwar Ibrahim wakipongeza mawaziri wao wa mambo ya kigeni baada ya kutia saini makubaliano n a mataifa ya ASEAN, Jumapili mjini Tokyo, Japan

Viongozi wa Japan pamoja na ushirika wa mataifa ya Asia Kusini Mashariki katika kikao maalum Jumapili, kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 50 ya urafiki wao.

Waliohudhuria wamepitisha mtizamo wa pamoja ambao unasisitiza ushirikiano wa kiusalama na kiuchumi wakati wakiheshimu utawala wa sheria huku mivutano ikiongezeka na China kwenye maji ya bahari ya kieneo.

Waziri mkuu wa Japan Fumio Kishida pia amefanya mfululizo wa mazungumzo ya pamoja na viongozi wa muungamo huo wa ASEAN, Jumamosi, na kutia saini makubaliano ya kutoa misaada ya kijeshi kwa Malaysia na Indonesia, ili kuongeza uwezo wao usalama wa baharini.

Japan imeweka umuhimu wa kuimarisha ushirikiano katika nyanja za usalama na ulinzi, wakati ikiboresha msaada kwa juhudi za ASEAN kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa na uwekezaji, ikiwa ni pamoja na sekta ya magari, Kishida amesema.

Forum

XS
SM
MD
LG