Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 22, 2024 Local time: 14:12

Jamii ya Kimataifa yalaumiwa kwa maafa Somalia


Mama na mwanawe aliyedhoofishwa na njaa
Mama na mwanawe aliyedhoofishwa na njaa

Wasomali 260,000 walipoteza maisha kutokana na njaa mwaka wa 2010-2012.Vifo ambavyo vingezuilika kwa msaada wa dharura wa jamii ya kimataifa

Uchunguzi juu ya baa la njaa la hivi karibuni nchini Somalia unatoa lawama kali kwa jamii ya kimataifa kwa kushindwa kuitikia kwa haraka mwito wa kuepusha taifa hilo na janga ambapo watu 260,000 walipoteza maisha yao.

Ripoti ya pamoja iliyoandaliwa na shirika la chakula na kilimo la Umoja wa Mataifa na lile la Marekani linalochunguza uwezekano wa njaa na kutoa onyo mapema, inakisia kuwa baa la njaa Somalia mwaka wa 2010 hadi 2012 liliuwa watoto 133,000 wa chini ya miaka mitano.

Huu ni uchunguzi wa kwanza wa kisayansi juu ya janga hilo.Ripoti za hapo awali zilikisia kuwa maelfu ya wasomali walikufa kutokana na njaa.

Phillippe Lazzarini mratibu wa maswala ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia maswala ya Somalia anasema idadi hiyo hiyo inashtua. Alisema jamii ya kimataifa ingelichukua hatua bora zaidi kuzuia baa hilo la njaa, maisha ya wasomali wengi yangeliokolewa.
XS
SM
MD
LG