Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 03, 2023 Local time: 19:49
VOA Direct Packages

Israel yaongeza shambulizi lingine Damascus mapema Jumanne


Picha ya maktaba ya shambulizi la roketi ya Israel mjini Damascus, Syria.

Shambulizi la anga la Israel  limeulenga  mji mkuu wa Syria,Damascus mapema  Jumanne kulingana na ripoti ya chombo cha habari cha  serikali likiwa la nne mjini humo tangu Alhamisi wiki iliyopita.

Wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa zaidi ya muongo mmoja nchini Syria, Israel imefanya mamia ya mashambulizi nchini humo, ikilenga vikosi vinavyoungwa mkono na Iran na wapiganaji wa Hezbollah wa Lebanon, pamoja na jeshi la Syria.

Chombo cha habari cha serikali ya Syria, SANA, kimesema kwamba mfumo wake wa ulinzi wa anga umenasa makombora kadhaa kwenye anga ya Damascus, akiashiria mashambulizi kutoka Israel. Hata hivyo awali chombo hicho kiliripoti sauti ya mlipuko karibu na Damascus.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Syrian Observatory for Human Rights linalofuatilia mapigano nchini humo limesema kwamba silaha za Israel zimekuwa zikilenga kituo cha Iran kilichoko karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Damascus.

XS
SM
MD
LG