Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 01, 2023 Local time: 17:50

Israel yaongeza muda wa kusitisha mapigano kwa saa 24


Mama wa Kipalestina akionesha poicha za vijana wake walouliwa wakati wa mashambulizi ya Israel huko Gaza.

Baraza la mawaziri la Israel limekubali ombi la Umoja wa Mataifa kuongeza muda wa kusitisha mapigano kwa saa 24, baada ya muda wa saa 12 kumalizika Jumamosi.

Mwanajeshi wa Israel asimama juu ya kifaru nje ya Ukanda wa Gaza, Julai 26, 2014.
Mwanajeshi wa Israel asimama juu ya kifaru nje ya Ukanda wa Gaza, Julai 26, 2014.

Afisa wa serikali ya Israel amesema, mashambulio yatasitishwa hadi saa sita za usiku Juampili, lakini Israel itajibu shambulio lolote la roketi litakalofanywa na wapiganaji wa Hamas, na kuendelea kutafuta na kuharibu njia za chini kwa chini huko Gaza.

Viongozi wa Hamas wamekata kutambua muda huo uloongezwa wakidai kuondolewa kwanaza wanajeshi wa Israel kutoka Gaza. Wapiganaji wa Hamas walifyetua roketi kadhaa ndani ya Israel mara baada ya muda wa awali wa saa 12 kumalizika Jumamosi lakini majeshi ya Israel hayakujibu.

Mpalestina akibeba vita vyake alivyopata baada ya nyumba take kubomolewa huko Beit Hanoun Julai 26, 2014.
Mpalestina akibeba vita vyake alivyopata baada ya nyumba take kubomolewa huko Beit Hanoun Julai 26, 2014.

Kusitishwa mapigano kwa muda siku ya Jumamosi kuliwapatia wakazi wa Gaza nafasi ya kurudi katika nyumba zao na kutizama kilichobaki kutokana na uharibifu mkubwa wa nyumba na mali ulofanywa na mashambulizi ya Israel.

Idadi ya wa-Palestina walouwawa hadi Jumamosi imepindukia elfu moja na waokozi waliweza kupata miili 100 wakati mapigano yaliposita. Wa-Israeli wamepoteza wanajeshi 37 na raia 2.

XS
SM
MD
LG