Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Mei 31, 2024 Local time: 00:46

IMF yatoa mkopo wa dola milioni 456 kwa Msumbiji


Alama ya Shirika la kimataifa la Fedha Duniani IMF nje ya makao makuu ya jengo hilo.
Alama ya Shirika la kimataifa la Fedha Duniani IMF nje ya makao makuu ya jengo hilo.

Shirika la kimataifa la  fedha duniani-IMF siku ya  Jumanne limetoa mkopo wa dola milioni 456 kwa Msumbiji.

Hii ikiwa ni mara ya kwanza toka iliposimama kufanya hivyo miaka sita iliyopita, katika kipindi ambacho ilitokea kashfa iliyoitwa “deni la kujificha” ikihusisha serikali.

Kutolewa kwa makubaliano hayo kulitangazwa mwishoni mwa mwezi Machi. IMF imesema kwamba fedha hizo zitasaidia kuokoa uchumi, na juhudi zinafanyika kupunguza deni la umma na kudhoofika kwa hali ya kifedha.

Amesema program hiyo inaiwezesha serikali kufanya mipango ya mabadiliko. Mwaka 2016 kulitokea kashfa kubwa ya ubadhirifu wa fedha kiasi cha Euro bilioni mbili.

XS
SM
MD
LG