Huku ikiwa na idadi ya watu milioni 12, uchumi wa Burundi unategemea kwa kiasi kikubwa katika mapato ya kilimo, haswa kutoka kwenye chai na kahawa.
Ukuaji unatarajiwa kukua kwa haraka ukichangiwa na uzalishaji wenye nguvu katika kilimo, uwekezaji wenye tija, na mageuzi yanayoendelea shirika hilo limesema katika taarifa Jumatatu jioni .
Uhaba wa mafuta ulidumaza harakati za uchumi mwaka 2023, shirika hilo limesema.
Uchumi wa Burundi ndio unaanza kuimarika tena kutokana na mzozo wa miaka mingi na misukosuko ya kisiasa chini ya kiongozi wa zamani Pierre Nkurunziza ambayo iliacha sekta kuu zikiyumba.
Forum