Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 01, 2022 Local time: 01:36

Idara ya Uhamiaji ya Kenya yalaumiwa


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Wakenya wanatumia njia za mkato kupata stakabadhi wanazohitaji, na hilo ni hatari kwa usalama wa taifa.

Kwa kipindi kirefu wakenya hasa wakaazi wa eneo la Pwani wamelalamikia kunyanyaswa na idara za usajili wa watu na ile ya uhamiaji wakati wa kutoa vitambulisho vya kitaifa, vyeti vya kuzaliwa au hati za kusafiria.

Kutokana na malalamiko hayo tume ya utekelezaji haki imefanya uchunguzi na kutoa ripoti kuhusu chanzo cha matatizo hayo na kutishia usalama wa taifa hilo.

Taarifa zinasema kwenye ripoti hiyo ni asilimia 2.8 ya wakenya wanaridhika na huduma zinazotolewa na idara ya kutoa vitambulisho na uhamiaji , idara ambazo zinawafanya wakenya kukosa stakabadhi halisi za kujitambulisha.

Naibu mwenyekiti wa tume hiyo Regina Muatha amesema kuwa hatua hiyo imesababisha wakenya kutumia njia za mkato kupata stakabadhi hizo suala ambalo ni hatari kwa usalama wa taifa.

XS
SM
MD
LG