Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 23, 2024 Local time: 08:52

Idadi ya vifo katika jengo Tanzania yaongezeka


Waokozi wakitoa mmoja wa watu waliokutwa wamekufa katika kifusi cha jengo hilo
Waokozi wakitoa mmoja wa watu waliokutwa wamekufa katika kifusi cha jengo hilo
Maafisa nchini Tanzania wamesema Jumatatu kuwa idadi ya watu waliokufa katika ajali ya kuanguka kwa jengo lililokuwa katika ujenzi mjini Dar es salaam Ijumaa iliyopita imefikia 36. Watoto kadha ni miongoni mwa waliofariki.

Maafisa wanasema watu wasiopungua 18 wameokolewa wakiwa hai katika jengo hilo la ghorofa 16 ambalo lilikuwa katika viwango vya mwisho mwisho vya ujenzi.

Waokoaji wamekata tamaa kuokoa watu zaidi wakiwa hai katika vifusi. Idadi kamili ya watu waliokuwa ndani ya jengo hilo na ujirani wake haifahamiki kwa hakika, na inaaminika kuwa wengi zaidi watakuwa wamekufa.

Maafisa wanasema wanachunguza sababu za kuanguka kwa jengo hilo na wamewashikilia watu wanne kwa mahojiano. Kuanguka kwa majengo ni kitu kinachotokea mara kwa mara katika mataifa ya Afrika, hasa kutokana na viwango hafifu vya ujenzi.
XS
SM
MD
LG