Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 26, 2025 Local time: 18:25

HRW inasema kuna pazia zito la ghasia linazunguka uchaguzi Nigeria


Tume huru ya uchaguzi Nigeria (INEC) ikichambua kadi maalum ya wapiga kura (PVC) mjini Lagos, Nigeria, Jan. 12, 2023.
Tume huru ya uchaguzi Nigeria (INEC) ikichambua kadi maalum ya wapiga kura (PVC) mjini Lagos, Nigeria, Jan. 12, 2023.

Ghasia hizo "zinadhoofisha haki za msingi za watu kupiga kura," alisema Anietie Ewang mtafiti wa Human Rights Watch nchini Nigeria ambaye alitoa wito kwa maafisa wa Nigeria kuweka mifumo salama itakayowawezesha Wa-Nigeria kupiga kura kwa  salama

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema jumatatu kwamba kuna "pazia zito la ghasia" zinazozunguka uchaguzi uliopangwa kufanyika nchini Nigeria baadaye mwezi huu.

Ghasia hizo "zinadhoofisha haki za msingi za watu kupiga kura," alisema Anietie Ewang, mtafiti wa HRW wa Nigeria, ambaye alitoa wito kwa maafisa wa Nigeria kuweka mifumo salama itakayowawezesha Wa-nigeria kupiga kura kwa salama.

"Ni muhimu kwa mamlaka kurejesha haraka imani ya umma kwa uwezo wao wa kuwawajibisha wale wanaohusika na vurugu za uchaguzi na kuhakikisha usalama wa Wanigeria wote," Ewang alisema katika taarifa.

Katika mji mkuu wa jimbo la Imo, Owerri, ambako makundi ya watu wanaotaka kujitenga yamekuwa yakishambulia mara kwa mara mamlaka za uchaguzi katika juhudi za kuvuruga uchaguzi, mwanaharakati mmoja wa haki za binadamu ameliambia shirika la HRW kwamba watu wanataka kupiga kura kuwa sehemu ya mchakato wa kisiasa, "lakini hili linapingwa vikali na masuala ya usalama ambapo inaonekana kuwa na dhamira ndogo ya kulielezea au hakuna kabisa."

XS
SM
MD
LG