Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 28, 2023 Local time: 21:46

Hospitali ya Bukavu kupatiwa umeme unaotumia nguvu za jua


Kina mama wakiwa na watoto wao katika moja ya hospitali za DRC

Suntech inachangia kiasi cha dola 500,000 na Global Echo inachangia kiasi cha dola 150,000 zilizohitajika kwa ajili ya vifaa maalumu

Taasisi ya Echo Global yenye makao yake Uingereza imetangaza kuwa inashirikiana na kampuni ya China ya Suntech kuipatia hospiali moja mashariki mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo umeme unaotumia nguvu za jua.

Philippe Cousteau Jr, mwanzilishi mwenza wa Global Echo aliiambia sauti ya Amerika-VOA kuwa mradi huo utaisaidia hospitali ya Panzi kushughulikia matatizo yake kulingana na gharama na nishati isiyotabirika.

Hospitali hiyo iliyopo Bukavu ina utaalamu wa kutoa tiba kwa kinamama hasa wale waliotaabika kutokana na uzazi na matatizo yatokanayo na ghasia za ngono.

Causteau alisema hospitali hiyo inatumia mchanganyiko wa mafuta, mkaa, umeme na diseli na kwamba kutumia umeme wa nguvu za jua ambao utakuwa na faida kifedha na kimazingira.

Suntech inachangia kiasi cha dola 500,000 kwa vifaa maalum ambavyo vitatumika kutoa umeme unaotumia nguvu za jua kwa mradi huu. Kampuni hiyo inasema vifaa hivyo vitatoa hadi kilowati 300 za umeme.

Global Echo inachangia kiasi cha dola 150,000 zilizohitajika kwa ajili ya vifaa, ubunifu na utekelezaji na inafanya kazi kuzishawishi kampuni nyingine kutoa kiasi kingine cha dola 250,000 ili kukidhi gharama hizo.

Taasisi hiyo inapata fedha kutoka mfuko wa fedha za uwekezaji wa Global Echo ambao ulizinduliwa mwanzoni mwa mwaka huu kwa mkakati wa uwekezaji katika makampuni ambayo yana mtazamo wenye matumaini katika teknolojia, jamii au mazingira duniani.
XS
SM
MD
LG