Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 08:20

Hali ingali ni ya wasi wasi Sudan Kusini


Maisha ya wakazi wa Sudan Kusini yamebadilika kutokana na mapigano ya kikabila yanayoendelea nchini humo
Maisha ya wakazi wa Sudan Kusini yamebadilika kutokana na mapigano ya kikabila yanayoendelea nchini humo
Kundi la madaktari wasio na mipaka MSF, linasema wapiganaji nchini Sudan Kusini wameharibu na kufanya wizi katika mahospitali kwa kile ambacho kinaelezewa matukio ya kusikitisha dhidi ya vifaa vya afya, wafanyakazi na wagonjwa tangu mzozo uzuke nchini humo mwezi Disemba mwaka jana.

Katika taarifa iliyotolewa jumatano kundi hilo lilisema timu hiyo imegundua miili 14 katika hospitali moja siku ya jumamosi mjini Malakal na miili mingine kadhaa ikionyesha kuwa walikuwa wagonjwa ambao walipigwa risasi wakiwa vitandani.

Malakal ni mji mkuu wa jimbo la Upper Nile na umekuwa ni eneo la mapigano makali kati ya majeshi ya serikali na waasi. Pande hizo mbili zilipigana wiki iliyopita licha ya kutiwa saini kwa sitisho la mapigano ambalo lilifikiwa Ethiopia mwezi uliopita.

Afisa wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Toby Lanzer ameiita hali ya Upper Nile si thabiti hata kidogo wakati alipolitembelea eneo hilo jumatano.

Madaktari wasio na mipaka wamesema hospitali ya Malakal ilikumbwa na wizi na wadi zake nyingine kuchomwa moto.

Katika jimbo la karibu la Unity kundi hilo lilisema wafanyakazi wake wamegundua tukio la kutisha sana katika hospitali ya Leer ambako majengo na vifaa vimechomwa moto, wakati madawa, vitanda vya wagonjwa na bidhaa nyingine kuibiwa.
XS
SM
MD
LG