Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 02:56

Ghasia zazuka katika bunge la Nigeria


Spika wa Bunge la Nigeria Aminu Tambuwal
Spika wa Bunge la Nigeria Aminu Tambuwal

Ghasia zimezuka katika Bunge la taifa nchini Nigeria alhamisi baada ya maafisa wa usalama kujaribu kumzuiya spika wa Bunge la wawakilishi kuingia katika eneo la Bunge.

Polisi imeiambia Sauti ya Amerika kwamba ilifyatua gesi ya machozi wakati wa ghasia hizo baina ya majeshi ya usalama na takriban wafuasi 200 wa spika Aminu Tambuwal.

Tambuwal alikikasirisha chama tawala cha People’s Democratic Party baada ya hivi karibuni kuhamia chama cha upinzani cha All Progressive Congress.

Magazeti ya Nigeria yanaripoti kuwa dazani ya maafisa wa idara ya usalama ya Nigeria walichukua udhibiti wa Bunge kabla ya kikao cha Alhamisi ambacho Tambuwal alitakiwa kukiendesha.

Taarifa zinasema spika alizuiwa kuingia ndani lakini Wabunge wengine waliingilia kati, wakaharibu mlango mkuu na kumuingiza Tambuwal ndani ya eneo hilo.

XS
SM
MD
LG