Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Machi 02, 2024 Local time: 04:16

Ghana yafufua matumaini yake kundi C


Asamoah Gyan wa Ghana (kushoto) akiwachia shuti lililoipa Ghana ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Algeria
Asamoah Gyan wa Ghana (kushoto) akiwachia shuti lililoipa Ghana ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Algeria

Kwa ushindi huu Ghana imefanikiwa kufufua matumaini yake ya kusonga mbele katika robo fainali ya fainali za kombe la Afrika 2015

Iliichukua Ghana mpaka dakika za majeruhi kufufua matumaini yake ya kuingia raundi ya pili ya fainali za kombe la mataifa Afrika huko Mongomo, Equatorial Guinea, kwa goli safi la juhudi kutoka kwa Asamoah Gyan . Ushindi huo wa 1-0 bila dhidi ya Algeria umeiweka Ghana katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu, sawa na Algeria na Senegal.

Baada ya kufungwa 2-1 na Senegal katika mechi yake ya ufunguzi Ghana ilikuwa inahitaji ushindi katika mechi yake na Algeria na hadi dakika 90 ilikuwa wazi kuwa matumaini ya Ghana yanazidi kudidimia.

Lakini pasi iliyotoka Mubarak Wakaso kepteni wa Ghana Gyan alimtoka mlinzi wa Algeria kwa mbio zilizoonyesha juhudi kubwa na kuachia mkwaju pembeni kwa mikono ya golikipa wa Algeria.

Kwa matokeo hayo kundi C ambalo linajulikana kama kundi la kifo lina timu tatu zenye pointi tatu kila moja zikiongozwa na Senegal, Ghana katika nafasi ya pili na Algeria katika nafasi ya tatu. Timu zote bado zina nafasi ya kuweza kuingia raundi ya robo fainali.

XS
SM
MD
LG