Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 17:03

Gary Johnson ameshinda uteuzi wa chama chake kuelekea uchaguzi mkuu Marekani


Mgombea urais Marekani wa chama cha Libertarian, Gary Johnson.
Mgombea urais Marekani wa chama cha Libertarian, Gary Johnson.

Mlibertarian Gary Johnson ambaye alikuwa hajulikani sana katika siasa za Marekani kwa mara nyingine ameshinda uteuzi cha chama chake siku ya Jumapili na kuleta mtizamo mpya katika ugombea wake wakati wamarekani wengi wana maoni yasiyo mazuri kwa wagombea wa vyama viwili vikuu, mrepublican Donald Trump na mdemocrat Hillary Clinton.

Ukusanyaji maoni wa karibuni ulionyesha kuwa Johnson mwenye umri wa miaka 63 ambaye alitumika katika vipindi viwili kama gavana wa Republican katika jimbo la kusini magharibi la New Mexico kuanzia mwaka 1995 mpaka 2003 kabla ya kuwa mlibertarian anashinda kwa kiasi cha asilimia 10 ya kura kitaifa dhidi ya Trump na Clinton kinadharia katika ushindani wa wagombea watatu hapo mwezi November.

Gavana wa zamani wa Massachusetts, William Weld siku ya Jumapili alichaguliwa kuwa mgombea mwenza wa Johnson, uteuzi huo ulifanywa kwenye mkutano wa Libertarian uliofanyika Orlando, katika jimbo la Florida siku ya Jumapili.

XS
SM
MD
LG