Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Mei 19, 2024 Local time: 18:16

Kenya yapata Mwanamke wa Kwanza Kuendesha Feri


Mishi Idi Omar, nahodha wa Feri huko Likoni, Mombasa.
Mishi Idi Omar, nahodha wa Feri huko Likoni, Mombasa.

Mishi ni mwanamke wa kwanza nchini Kenya kuwa nahodha wa Feri.

Licha ya kuzaliwa katika jamii ambayo imemtambua mwanamke kama “mtu wa jikoni” na ikiwa ni kazi afanye za kike, Mishi Idi Omar ameweka historia nchini Kenya kwa kuwa mwanamke wa kwanza kuwa nahodha wa feri, usafiri unaotumiwa na maelfu ya wenyeji wa pwani na hata wasafiri kutoka nchi jirani ya Tanzania.

Akiwa mkaazi na mzaliwa wa Likoni huko Mombasa nchini Kenya, mara nyingi akitumia feri kuvuka hadi Mombasa Kisiwani, Mishi aliye na umri wa miaka 36 ametimiza ndoto yake kuwa nahodha wa feri.

Sasa yeye ni mwanamke wa kwanza kuendesha feri nchini Kenya.

please wait

No media source currently available

0:00 0:05:30 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Mishi Omar -mama wa watoto wawili alisomea utaalamu wa maabara katka chuo kikuu cha Mombasa, (Labarotaory technologist), mara tu baada ya kukamilisha masomo ya sekondari.

Hata hivyo baada ya kumaliza shahada yake ya utaalamu wa maabara na kufanya kazi katika vituo vya afya, Mishi alijiunga na shirika la feri mwaka 2005 kama baharia (kwa kimombo Dekand), katika harakati ya kutafuta kazi.

Kwa kutumia kivuko cha likoni katika harakati zake za kila siku, ni miongoni mwa sababu zilizomvutia kuwa nahodha.

Na licha ya kuwa mwanamke wa pekee kati ya manahodha 26 wanaohudumia shirika la Kenya Ferry, Mishi anasema haoni tofauti katika utendaji wake wa kazi.

Jamii anayotoka imekuwa na itikadi za kuchagua kazi kulingana na jinsia,.

Na huku feri ikivusha maelfu ya watu na magari, na kutokana na changamoto ambazo hukumba feri kimitambo, Mishi anaeleza kuwa uzoefu wa kazi yake , unampa nguvu ya kuendesha chombo hicho kuhakikisha usalama wa maelfu ya abiria.

XS
SM
MD
LG