Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 04, 2024 Local time: 17:19

Fedha za kusaidia familia masikini DRC, zadaiwa kuibwa


Wakazi wa DRC wanaotoroka mapigano, kwenye picha ya maktaba.
Wakazi wa DRC wanaotoroka mapigano, kwenye picha ya maktaba.

Shirika moja la kutoa misaada la Marekani limedai kuwa takriban dola 900,000 ziliibwa kutoka kwenye mradi wake huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo Congo na baadhi ya wafanyakazi wake wakishirikiana na watu wa nje.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, shirika hilo kwa jina GiveDirectly, liligundua kuwa baadhi ya wafanyakazi wake nchini Congo walishirikiana na watu wa nje kuvuja fedha zilizolenga kusaidia zaidi ya familia masikini 1,700 ndani ya kipindi cha miezi 6 kuanzia Agosti 2022.

Taarifa zimeongeza kusema kwamba fedha hizo zilipotea baada ya kubadili mfumo wa ulipaji, ili kufikia vijiji vilivyokuwa maeneo ya ndani yasio kuwa na usalama.

Shirika hilo limeongeza kusema kwamba uchunguzi unaendelea ambapo sehemu ndogo ya fedha zilizo ibwa imepatikana, ingawa huenda nyingi zisipatikane. Hata hivyo wameongeza kusema watahakikisha kuwa familia ziliazoathiriwa zitapata misaada yao licha ya wizi huo.

Forum

XS
SM
MD
LG