Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 25, 2024 Local time: 23:04

Ethiopia yashinda medali ya dhahabu katika mashindano ya Olimpiki


Selemon Barega wa Ethiopia akishangilia na bendera ya nchi yake baada ya kutwaa medali ya dhahbu mita 10000.
Selemon Barega wa Ethiopia akishangilia na bendera ya nchi yake baada ya kutwaa medali ya dhahbu mita 10000.

Selemon Barega wa Ethiopia ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 10000  wanaume

Selemon Barega wa Ethiopia ameshinda medali ya dhahabu katika mbio za mita 10000 wanaume wakati waafrika walitawala mbio hizo kwenye uwanja wa Olimpiki wa Tokyo Ijumaa. Barega amewashinda wengine kwa mita chache za mwisho kumaliza kwa dakika 27, sekunde 43.22 mbele ya Joshua Cheptegei wa Uganda aliyetwaa medali ya fedha kwa muda wa dk.27: 43.63 wakati mwenzake Jacob Kiplimo alitwaa medali ya shaba akitumia muda wa dk. 27: 43.88.

Berihu Aregawi wa Ethiopia alimaliza wa nne akitumia muda wa dk.27: 46.16. Waafrika wengine watatu walimaliza katika kumi bora. Rogers Kwemoi wa Kenya alishika nafasi ya saba kwa dakika 27: 50.06 akifuatiwa katika nafasi ya nane na Yomif Kejelcha wa Ethiopia aliyemaliza akitumia muda wa dk 27: sekunde 52.03. Rhonex Kipruto wa Kenya alimaliza wa tisa akitumia dk. 27: sekunde 52.78.

XS
SM
MD
LG