Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 05, 2022 Local time: 17:50

Dunia yaukaribisha mwaka 2013


Fataki zikirushwa huko Sydney, Australia kusheherekea mwaka mpya.
Fataki nyingi zimerushwa kwenye bandari ya Sydney, Australia na mataifa mengine ya Pacific yamekuwa ya kwanza kuukaribisha mwaka mpya wa 2013 .

Kiasi cha watu milioni 1.5 walizunguka bandari ya Sydney na kuona maonyesho ya fataki zilizo gharimu dola milioni 6.9 huku wengine wakipiga kambi nje kwa karibu siku nzima ili kupata nafasi ya kujionea sherehe hizo vizuri. Watu wengi zaidi walifuatilia matukio haya kwenye televisheni duniani kote wakati nyota wa muziki wa Australia, Kylie Minogue alipobonyeza kitufe cha kuanza sherehe za mwaka mpya huku wimbo wake ukipigwa na watu wakichezwa.

Huko Japan mamilioni ya watu walikuwa wakitembelea nyumba ya sala ya Shinto na hekalu la wabudha kwa sherehe za mwisho za kuaga mwaka 2012 na kuukaribisha mwaka 2013. Na nchini Marekani tungali saa chache nyuma watu wakisubiri pia kuukaribisha mwaka mpya kwa kujumuika pamoja kwenye sherehe mbalimbali.
XS
SM
MD
LG