Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 20, 2024 Local time: 11:42

Donald Trump aongoza jimbo la Nevada


Kutoka kushoto ni Marco Rubio, Donald Trump na Ted Cruz.
Kutoka kushoto ni Marco Rubio, Donald Trump na Ted Cruz.

Bilionea Donald Trump alishinda jimbo jingine kwa ushindi mkubwa katika kinyang’anyiro chake cha kuwania uteuzi wa urais wa Republican hapo Jumanne katika jimbo la Nevada nchini Marekani.

Matokeo ya mwisho yalionesha kwamba Trump alipata asilimia 46 ya kura akiwa mbele ya seneta wa Florida, Marco Rubio aliyepata asilimia 24. Seneta wa Texas, Ted Cruz alishika nafasi ya tatu kwa kupata asilimia 21.

Donald Trump
Donald Trump

Trump ameshinda mara tatu mfululizo kwa ushindi mkubwa baada ya kupata ushindi katika uchaguzi wa awali uliofanyika huko katika jimbo la New Hampshire na South Carolina mwanzoni mwa mwezi huu.

Ushindi huu pia unampa hamasa ya kusonga mbele kuingia katika wiki muhimu kwenye kampeni za uchaguzi akiwa na darzeni ya kura za majimbo kwenye Super Tuesday inayotarajiwa kufanyika Machi mosi.

XS
SM
MD
LG