Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 06:35

CUF bado yapigania mageuzi miaka 13 baada ya ghasia za Zanzibar


Maandamano ya wafuasi wa CUF wakati wa kampeni za uchaguzi wa 2005 Zanzibar
Januari 26 na 27 ya kila mwaka chama cha upinzani cha wananchi CUF, huadhimisha kumbukumbu ya maandamno ya kudai demokrasia zaidi katika visiwani Zanzibar yaliyofanyika mwaka 2001. Wafuasi kadhaa wa chama hicho waliuwaa na wengine kujeruhiwa katika maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 katika mapambano na polisi.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2000 katika visiwa vya zanzibar uligubikwa na utata uliozusha vurugu kubwa na maandamano kutoka chama cha CUF kikidai kuporwa ushindi wao katika uchaguzi uliomweka madarakani wakati huo, Rais Aman Abeid Karume hivyo kutaka urudiwe..
please wait
Embed

No media source currently available

0:00 0:02:23 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Kamati maalum iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania wakati huo Benjamn Mkapa kuhusiana na uchunguzi wa vurugu hizo iliyoongozwa na Brigedia Jenerali Hashim Mbita, ilibaini kwamba watu takribani 23 walipoteza maisha wakati wa maandamnao hayo ya wafuasi wa CUF ambapo pia kwa mara ya kwanza Tanzania ilizalisha wakimbizi kwa baadhi ya watu kukimbilia mjini Mombasa na kwingineko kukwepa vuruga hizo.

Akizungumza na Sauti ya Amerika jijini Dar es salaam Jumatatu Mkurugenzi wa Mipango, Uchaguzi na Bunge wa chama cha wananchi CUF, Shaweji Mketto, alikumbusha kwanza madai ya chama hicho wakati huo ambayo amesema pia bado wanaendelea kuyapigania hadi leo, nayo ni uchaguzi huru na wa haki..

Aidha CUF imewakumbusha watanzania umuhimu wa kumbukumbu hii ya kudai demokrasia zaidi nchini hususan wakati huu ambapo Tanzania ipo katika mchakato wa kudai katiba mpya itakayohakikisha kuwepo kwa tume huru ya uchaguzi...

Serikali ya umoja wa kitaifa visiwani Zanzibar iliyoundwa baina ya vyama vya CCM na CUF baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 ni moja ya matunda ya maridhiano baina ya vyama hivyo kufuatia mlolongo wa migogoro ya kisiasa iliyokuwa ikiibuka kila baada ya uchaguzi na ndipo vyama hivyo kupitia rais wa wakati huo Aman Abeid Karume kufanya mazungumzo ya muafaka wa kisiasa na katibu mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad
XS
SM
MD
LG