Wakosoaji wanasema kwamba utawala huo unajaribu kudhibiti utaoaji wa habari wakati ukikabiliwa na ukosefu mkubwa wa usalama nchini. Burkina Faso imekuwa taifa la pili baada ya Mali kusitisha utangazaji wa RFI, wakati mataifa yote mawili yakiwa chini ya utawala wa kijeshi.
Muda mfupi baada ya tangazo hilo kufanywa mwishoni mwa wiki, RFI kupitia taarifa ililalamikia hatua hiyo na kusema kwamba ingefanya kila juhudi kuhakikisha kuwa matangazo yake yanarejeshwa.
Taarifa kutoka utawala wa kijeshi wa Burkina Faso ilisema kwamba RFI ilitoa taarifa za kupotosha kuhusiana na madai ya jaribio la mapinduzi wiki iliyopita, na kuwapa sauti wapiganaji wa kiislamu.