Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:11

Bunge la Malaysia limepitisha mswada kuondoa hukumu ya kifo


Naibu waziri wa Sheria Malaysia, Ramkarpal Singh, (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari.
Naibu waziri wa Sheria Malaysia, Ramkarpal Singh, (Kulia) akizungumza na waandishi wa habari.

Malaysia imekuwa ikidhibiti kwa muda hukumu za kunyongwa tangu mwaka 2018, lakini mahakama zimeendelea kuwapeleka wafungwa katika hukumu ya kifo

Bunge la Malaysia limepitisha mswaada Jumatatu wa kuondoa hukumu za lazima za vifo huku makundi ya kutetea haki za binadamu yakikaribisha kura hiyo kama hatua muhimu ambayo inaweza kufanyika kwingineko Asia Kusini Mashariki.

Hukumu kwa makosa kadhaa, ikiwa ni pamoja na mauaji na biashara ya dawa za kulevya hapo awali ilikuja na adhabu ya kifo moja kwa moja na kuwapa majaji fursa ya kutekeleza hilo.

Mswada huo haufuti hukumu ya kifo lakini badala yake unawapa majaji fursa pana ya kutoa adhabu ya kifungo cha muda mrefu kati ya miaka 30 hadi 40 chini ya masharti fulani. Akizungumza mbele ya baraza dogo la bunge la Malaysia, Naibu Waziri wa Sheria Ramkarpal Singh alisema hatuwezi kupuuza kiholela uwepo wa haki ya asili ya kuishi ya kila mtu.

Malaysia imekuwa ikidhibiti kwa muda hukumu za kunyongwa tangu mwaka 2018, lakini mahakama zimeendelea kuwapeleka wafungwa katika hukumu ya kifo. Mageuzi hayo bado yatalazimika kupelekwa kwenye baraza la seneti lakini yanatarajiwa kupita bila upinzani mkubwa.

XS
SM
MD
LG