Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Aprili 24, 2024 Local time: 00:47

Rotich ashinda Boston Marathon


Mbio za Boston Marathon, April 20, 2015
please wait

No media source currently available

0:00 0:01:14 0:00

Mwanadada wa Kenya Caroline Rotich aliibuka mshindi wa mbio ndefu za Boston marathon Jumatatu baada ya kumshinda mpinzani wake mkubwa Mare Dibaba wa Ethiopia katika mita 100 za mwisho za mbio hizo.

Rotich alitia fora mbele ya maelfu kwa maelfu ya watazamaji pale alipochanganya miguu na kumaliza kwa kasi katika muda wa saa mbili, dakika 24 na sekunde 55.

Meya wa Boston Marty Walsh akimvalisha taji Caroline Rotich wa Kenya l 20, 2015 in Boston. (AP Photo/Elise Amendola)
Meya wa Boston Marty Walsh akimvalisha taji Caroline Rotich wa Kenya l 20, 2015 in Boston. (AP Photo/Elise Amendola)

Kwa upande wa wanaume Lelisa Desisa wa Ethiopia ambaye alishinda mbio hizo mwaka jana na kurejesha medali yake kwa mji wa Boston baada ya mashambulizi ya mabomu alirudia tena ushindi wake na kuchukua nafasi ya kwanza katika muda wa saa mbili, dakika 9 na sekunde 17,

Yemane Adhane Tsegay wa Ethiopia alichukua nafasi ya pili katika muda wa saa mbili, dakika 9 na sekunde 48 wakati Mkenya Wilson Chebet alishinda nafasi ya tatu katika muda wa saa mbili, dakika 10 na sekunde 22.

Lelisa Desisa mshindi wa Boston marathon kwa wanaume
Lelisa Desisa mshindi wa Boston marathon kwa wanaume

Tukirudi kwa upande wa wanawake Buzunesh Deba pia wa Ethiopia alishinda nafasi ya tatu katika muda wa saa mbili, dakika 25 na sekunde 09.

Mbio za wanawake zilikuwa na msisimko mkubwa huku wanawake watano wakiwa wanapambana bega bega kwa muda mrefu hadi kilomita za mwisho pale Dibaba, Rotich na Deba waliwapowatoka wenzao na kufanya mashindano baina yao wenyewe.

Katika dakika za mwisho Dibaba alisonga mbele ya Rotich na ilielekea atashinda mbili hizo lakini Rotich alivuta nguvu zake zote za kumtoka Dibaba katika dakika za mwisho kabisa.

XS
SM
MD
LG