Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 20, 2025 Local time: 09:38

Boko Haram na Ansaru yatajwa kuwa makundi ya kigaidi


Bango lenye picha ya kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau, katika kijiji cha Baga, Maiduguri.
Bango lenye picha ya kiongozi wa kundi la Boko Haram Abubakar Shekau, katika kijiji cha Baga, Maiduguri.
Marekani imeorodhesha makundi ya wanagambo wa Nigeria Boko na Ansaru kama makundi ya kigaidi ya kigeni.

Katika taarifa Jumatano afisa wa idara ya kupambana na ugaidi ya Marekani Lisa Manaco alisema makundi hayo mawili yamewajibika na vifo vya maelfu ya watu kaskazini mashariki na katikati mwa Nigeria katika miaka ya hivi karibuni.

Alisema makundi hayo yamefanya mashambulizi mengi katika makanisa na misikiti kuuwa raia. Marekani inashtumu Boko Haram kwa shambulizi la mwaka 2011 katika jengo la Umoja wa Mataifa mjini Abuja lililouwa watu 21.
XS
SM
MD
LG