Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 17:48

Bingwa mtetezi Nigeria ashindwa kufuzu katika kombe la Afrika


Nigeria iliyokuwa bingwa mtetezi wa kombe la mataifa ya Afrika imeshindwa kufuzu fainali za mwakani.
Nigeria iliyokuwa bingwa mtetezi wa kombe la mataifa ya Afrika imeshindwa kufuzu fainali za mwakani.

Michezo ya mwisho ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika imemalizika. Sasa orodha rasmi ya timu zitakazo shiriki fainali hizo zilizopangwa kufanyika kuanzia Januari 14 mwakani imepatikana.

Bingwa mtetezi Nigeria imeyaaga mashindano hayo kwa kushika nafasi ya tatu katika kundi A. Kwa hali hiyo fainali hizo za mwakani zitafanyika bila bingwa mtetezi Nigeria.

Michezo ya kundi A, Afrika Kusini imetoka sare ya 2-2 dhidi ya Nigeria, na Congo ikiifunga Sudan kwa 1-0. Afrika Kusini inasonga mbele kwa pointi 11, ikifuatiwa na Congo yenye pointi 10. Nigeria na Sudan zimeshindwa kufuzu.

Kundi B, Mali imeifunga Algeria 2-0 huku Ethiopia na Malawi zikishindwa kufungana. Kwa matokeo hayo, Aljeria imefuzu kwa kufikisha pointi 15 ikifuatiwa na Mali yenye pointi 9. Malawi na Ethiopia zimetoka rasmi.

Mashabiki wa Burkina Faso
Mashabiki wa Burkina Faso

Matokeo ya Kundi C, Burkina Faso imetoka suluhu na Angola ya 1-1 huku Gabon ikishinda 4-1 dhidi ya Lesotho. Burkina Faso inasonga mbele kwa pointi 10, ikifuatiwa na Gabon yenye pointi 9. Angola na Lesotho zimeaga mashindano.

Katika kundi D, Cameroon na Ivory Coast zimeshindwa kufungana, huku DRC Congo ikishinda 3-1 dhidi ya Sierra Leone. Cameroon imefuzu kwa pointi 14, ikifuatiwa na Ivory Coast kwa pointi 10. DRC Congo na Sierra Leone zimeaga mashindano.

Kwa upande wa kundi E, Ghana imeifunga Togo kwa 3-1 huku Guinea ikishinda 2-0 dhidi ya Uganda. Ghana imefuzu kwa pointi 11 ikiwa mbele ya Guinea yenye pointi 10. Uganda na Togo zimetupwa nje ya mashindano.

Kundi F limeongozwa na Cape Verde, japokuwa ilifungwa na Zambia 1-0. Niger imetoka suluhu na Msumbiji ya 1-1 na hivyo Cape Verde kufuzu kwa pointi 12 mbele ya Zambia yenye pointi 11. Msumbiji na Niger zimeshindwa kufuzu.

Kundi la mwisho G, Tunisia imeifunga Misri 2-1 na Senegal ikitoa kipigo cha 3-0 dhidi ya Botswana. Tunisia ikiwa na pointi 14 na Senegal yenye pointi 13 zinasonga mbele kwa pamoja. Botswana na Misri nazo sasa zimetupwa nje rasmi.

Timu zilizofuzu katika orodha ni Afrika Kusini, Congo, Algeria, Mali, Burkina Faso, Gabon, Cameroon, Ivory Coast, Ghana, Guinea, Cape Verde, Zambia, Tunisia na Senegal.

XS
SM
MD
LG