Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Mei 04, 2024 Local time: 17:43

Biden atembelea Helsinki kwenye hafla ya kuipongeza Finland kujiunga na NATO


Rais wa Marekani Joe Biden alipowasili mjini Helsinki Julai 13, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden alipowasili mjini Helsinki Julai 13, 2023.

Rais wa Marekani Joe Biden Alhamisi yupo mjini Helsinki, Finland, kwa mkutano na  viongozi wa mataifa ya Nordic yanayofahamika kama nchi za Scandinavia, ili kuipongeza Finland kwa kujiunga na NATO.

Ratiba ya Biden inajumuisha kikao na rais wa Finland Sauli Niinisto kabla ya kukutana na viongozi wengine wakiwemo waziri mkuu wa Sweden Ulf Kristersson, waziri mkuu wa Norway Jonas Gahr Store, waziri mkuu wa Denmrak Mette Frederiksen na waziri mkuu wa Iceland Kartin Jakobsdottir.

Kikao hicho cha Marekani na mataifa ya Scandinavia kinatarajiwa kuzungumzia masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa, ushirikiano wa usalama pamoja na teknolojia zinazoibuka. Finland na Sweden zilitoa ombi la kujiunga na NATO mwaka jana, baada ya Russia kuivamia Ukraine.

Finland na Sweden waliomba kujiunga na NATO ikiwa ni majibu ya uvamizi wa Russia huko Ukraine mwaka jana.

Muungano huo uliikaribisha Finland mwezi Aprili, lakini juhudi za Sweden zilichelewa baada ya Uturuki kulalamika kwamba Sweden imekuwa mpole sana kwa makundi ambayo Ankara yanayaona ni taasisi za kigaidi.

Forum

XS
SM
MD
LG