Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 28, 2024 Local time: 20:44

Bernie Sanders ashinda jimbo la West Virginia


Mgombea wa Republican, Donald Trump ameshinda majimbo yote mawili ya West Virginia na Nebraska.
Mgombea wa Republican, Donald Trump ameshinda majimbo yote mawili ya West Virginia na Nebraska.

Mitandao ya televisheni Marekani inabashiri kwamba seneta wa Vermont, Bernie Sanders amepata ushindi mdogo wa chama cha Democrat kwenye upigaji kura wa Jumanne wa uchaguzi wa awali katika jimbo la West Virginia dhidi ya waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Marekani, Hillary Clinton.

Seneta Sanders anatarajiwa kuongeza wajumbe wengine 13 lakini bado hana nafasi ya kumpita Clinton anayeongoza kuwa na idadi kubwa ya wajumbe. Mwanzoni mwa mwaka huu Clinton aliwakasirisha wapiga kura wengi wa jimbo la West Virginia wakati alipoamua kwamba hatoweka machimbo mengi ya makaa ya mawe na kuyaondoa kwenye biashara makampuni ya makaa ya mawe.

Mgombea urais wa Democrat, Hillary Clinton
Mgombea urais wa Democrat, Hillary Clinton

Makaa ya mawe ni hatari kwa migodi na ni chanzo cha nishati ya hewa chafu lakini baadhi ya sehemu za jimbo hilo zinategemea sana makaa ya mawe kwa ajili ya ajira na ushuru. Clinton aliomba radhi wiki iliyopita kwa wapiga kura wa jimbo la West Virginia akisema “ninataka ufahamu kwamba ninakwenda kufanya kila niwezalo ili kusaidia” wale walioathirika kutokana na kupunguzwa kwa madai ya makaa ya mawe.

Wakati huo huo hakukuwa na jambo la kushangaza kwa upande wa Republican kwenye uchaguzi wa Jumanne. Kama ilivyotarajiwa mgombea anayetarajiwa kupata uteuzi wa chama Donald Trump alishinda uchaguzi wa awali katika majimbo ya West Virginia na Nebraska huku akianza kumfikiria mtu anayemtaka kuwa mgombea mwenza wake katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.

Wapinzani wawili wa Trump katika kinyang’anyiro cha urais nchini Marekani walijitoa kwenye kampeni za kuwania uteuzi wa chama wiki iliyopita.

XS
SM
MD
LG