Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 18:53

Benjamin Netanyahu anatarajiwa kurudi madarakani Alhamis


Benjamin Netanyahu akizungumza huko Jerusalem hapo Nov. 2, 2022.
Benjamin Netanyahu akizungumza huko Jerusalem hapo Nov. 2, 2022.

"Hii ni mara ya sita ninaiwakilisha serikali ambayo ninaelekea kupata uungwaji mkono wa bunge, na ninafurahi kama mara ya kwanza," Netanyahu aliliambia bunge la Knesset kabla ya hafla ya kuapishwa"

Kiongozi mkongwe wa Israel Benjamin Netanyahu anatarajiwa kurejea madarakani Alhamisi baada ya kipindi kifupi cha upinzani, akiongoza kile wachambuzi wanachokiita serikali ya mrengo wa kulia zaidi katika historia ya nchi hiyo.

Netanyahu mwenye umri wa miaka 73 ambaye anapambana na mashtaka ya ufisadi mahakamani, tayari alihudumu kama Waziri Mkuu kwa muda mrefu kuliko mtu yeyote katika historia ya Israel ikiwa ni pamoja na kutoka mwaka 2009 hadi 2021 na kipindi cha miaka mitatu iliyopita mwishoni mwa miaka ya 1990.

"Hii ni mara ya sita ninaiwakilisha serikali ambayo ninaelekea kupata uungwaji mkono wa bunge, na ninafurahi kama mara ya kwanza," Netanyahu aliliambia bunge la Knesset kabla ya hafla ya kuapishwa.

Akikatizwa na wabunge wa upinzani wenye hasira, aliwaambia "Utawala wa kidemokrasia unajaribiwa na upande wake ulioshindwa kukubali uamuzi wa watu. Katika demokrasia inayofanya kazi, unaheshimu sheria za mchezo."

Netanyahu aliondolewa madarakani hapo Juni 2021 na muungano wa mrengo wa kushoto, wanasiasa wa mrengo wa kati na vyama vya Kiarabu vinavyoongozwa na Naftali Bennett na mtangazaji wa zamani wa habari wa televisheni Yair Lapid. Haikumchukua muda mrefu kurudi.

Kufuatia ushindi wake wa uchaguzi wa Novemba mosi, Netanyahu aliingia katika mazungumzo na vyama vya Ultra-Orthodox na vya mrengo mkali wa kulia.

XS
SM
MD
LG