Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 04:37

Australia na New Zealand zatathmini uharibifu ulioletwa na mlipuko wa volcano


Picha iliyochukuliwa kutoka angani inaonyesha boti zilizozama ikiaminika ziliathiriwa na mlipuko wa volcano uliotokana na tsunami, Japan. Kyodo/via REUTERS ATTENTION EDITORS -
Picha iliyochukuliwa kutoka angani inaonyesha boti zilizozama ikiaminika ziliathiriwa na mlipuko wa volcano uliotokana na tsunami, Japan. Kyodo/via REUTERS ATTENTION EDITORS -

Wanajeshi wa Australia na New Zealand wanatathmini uharibifu uliotokea kufuatia mlipuko mkubwa wa volcano wa chini ya Bahari ya Pacific kwenye Kisiwa cha Tonga siku ya Jumamosi.

Maafisa wamesema kwamba wamepokea ripoti kwa simu za satellite za kuwepo uharibifu kwa maduka na nyumba karibu na ufukwe wa bahari kutoka kwa watonga.

New Zealand imetuma msaada wa chakula na mahitaji muhimu ya kibinadamu, sawa na ndege za kuwahamisha watu kutoka sehemu hiyo.

Waziri Mkuu wa New Zealand Jacinda Ardern anasema: “Tayari tumetuma ndege za kufanya uchunguzi na za kuwapelekea msaada watu wa Tonga. Ndege hizo zimeelekea sehemu hiyo na zinatarajiwa kuteleza majiukumu yake bila kujali namna uwanja wa ndege ulivyo."

Australia, ambayo pia imetuma ndege za uchunguzi kwenye kisiwa hicho cha Tonga, imesema kwamba inashirikiana na maafisa wa sehemu hiyo katika kukabiliana na hali ilivyo.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Australia, Marise Payne, ameeleza: “Tutafanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Tonga, kwa ushirikiano na kamishna mkuu wa Tonga na Canbera ili kuhakikisha kwamba tunafikisha misaada inayohitajika kwa familia na marafiki wetu wa Pacific. Huu ni wakati wenye changamoto sana . mawasiliano ni mabaya sana kutokana na mlipuko wa Volcano.

Mlipuko wa Volcano, wa Hunga-Tonga-Hunga-Ha’apai, Jumamosi, uliharibu vibaya huduma za mawasiliano ya simu na internet kwenye kisiwa hicho.

Maafisa wa Tonga wanasema majivu ya Volcano yamesababisha hewa na maji ya kunywa kwenye kisiwa hicho kuchafuka na kuwasihi wakazi kuvaa barakoa na kutumia maji ya chupa.

XS
SM
MD
LG