Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 13, 2024 Local time: 22:12

Alshabaab wachukua udhibiti wa mji muhimu wa Merca.


Mwanamgambo wa Alshabab akiwa anaonyesha jambo kwa umma huko Elasha kusini mwa Mogadishu.
Mwanamgambo wa Alshabab akiwa anaonyesha jambo kwa umma huko Elasha kusini mwa Mogadishu.

Kundi la Wanamgambo wa Alshabab, limechukua udhibiti wa mji muhimu wa Merca, ulio umbali wa kilomita 100 Kusini mwa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Hayo ni kwa mujibu wa wakaazi na maafisa wa serikali. Vikosi vya serikali na vile vya kulinda usalama vya muungano AMISOM ambavyo vimekuwa vikiudhibiti mji huo viliondoka usiku wa manane na kuwaachia waasi wa Alshabab bandari moja katika pwani ya Somalia.

Mkaazi mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe aliiambia Sauti ya Amerika kwamba baada ya vikosi vya Amisom na wanajeshi wa serikali kuondoka, kwamba waasi wa Al-shabab waliokuwa wamejihami walishika doria na kukaa kwenye maeneo muhimu ya kuingia kwenye mji.

Na katika mahojiano na Sauti ya Amerika, Waziri wa Ulinzi wa jimbo la Kusini Magharibi mwa Somalia, Abdifita Ibrahim Geesey, alithibitisha kuwa wanamgambo hao wameudhibiti mji huo. Haya yanatokea baada ya wapiganaji wa Al shabab kudhibiti kwa muda kambi moja ya jeshi la serikali ya Somalia mjini Lanta Buur, uliokuwa jela hapo zamani, na ulikuwa umbali wa kilomita 40 Magharibi mwa Mogadishu. Kwa mujibu wa wakaazi na maafisa wa serikali, wanajeshi wanane na wanamgambo watano walipoteza maisha yao kufuatia makabiliano.

XS
SM
MD
LG